HOPE EMPOWERMENT AND DEVELOPMENT ORGANIZATION
Photo of Milford Sound in New Zealand!
Hope Empowerment And Development Organization
Nchini Kenya shirika moja limejitolea kuwasaidia akina mama waathiriwa wa HIV kuwanyonyesha watoto miezi sita mfululilzo

Dunia inaadhimisha wiki ya umuhimu wa kuwanyonyesha watoto. Mwaka huu mada kuu ni kutoa mazingira mazuri katika kuwasaidia wanawake kufanikisha jukumu hilo muhimu.
Nchini Kenya shirika moja limejitolea kuwasaidia akina mama waathiriwa wa HIV kuwanyonyesha watoto wao kwani wakati serikali inaposema akina mama wanyonyeshe miezi sita mfululilzo na wao wako katikan fungu hilo.

 sikiliza makala hii bofya hapo chini kusikiliza

http://wsodprogrf.bbc.co.uk/swahili/dps/2013/08/kenyabreasfeedingweekgood_130802_breasfeeding_week_au_bb.mp3

Zipo taarifa kwamba Serikali iko mbioni kubadilisha sera na miongozo yake kuhusu tiba na uchunguzi wa ugonjwa wa malaria ili dawa mpya ya Artesunate ianze kutumika kutibu malaria kali badala ya Quinine. Kwa vyovyote vile, taarifa hizo zitaleta mkanganyiko na hofu miongoni mwa wananchi, kwani hatua hiyo ya Serikali inaweza kutafsiriwa kwamba dawa ya Quinine imeshindwa kutibu ugonjwa huo sugu na kwamba imekuwa ikitumiwa tu kama majaribio.
Wasiwasi na hofu inayoweza kuwagubika wananchi kutokana na hatua hiyo ya Serikali inaeleweka. Kwanza, ugonjwa huo ndiyo unaoua watu wengi zaidi katika nchi maskini kama Tanzania kuliko ugonjwa mwingine wowote.
Hapa nyumbani, takwimu zinaonyesha kwamba watu wapatao 80,000 hufariki dunia kila mwaka na wengine milioni 12 huugua ugonjwa huo katika kipindi hicho. Kwa mujibu wa takwimu, asilimia 40 ya wagonjwa ambao huripoti katika vituo vya afya kila mwaka hufanya hivyo kwa kusumbuliwa na malaria.
Jambo la pili ni kwamba kubadilishwa kwa dawa hiyo ya Quinine na badala yake kutumia Artesunate kunaweza kutafsiriwa na wananchi wengi wa kawaida kwamba Quinine ambayo imekuwa ikitumika kwa miongo mingi imeshindwa kutibu ugonjwa huo. Hofu itakuja pale wananchi watakapoanza kujiuliza kuhusu madhara wanayoweza kuwa wameyapata kutokana na matumizi ya dawa hiyo.
Hapo ndipo zitakapoibuka hisia kwamba miili yao imekuwa ikitumika  muda wote huo kufanya majaribio ya dawa hiyo ya Quinine.
Ni jinsi gani basi wananchi watapokea ujio wa dawa hiyo ya Artesunate katika mazingira kama hayo ni swali linalosubiri wakati. Huko nyuma wananchi walishuhudia Serikali ikiziondoa sokoni dawa kadhaa za kutibu malaria moja baada ya nyingine, ikiwa ni pamoja na  Chloroquine, Fansida na Dawa Mseto (Alu), kwa maelezo kwamba vimelea vya ugonjwa huo vimekuwa sugu kwa dawa hizo. Unahitajika utafiti wa kutosha kabla dawa hazijapitishwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
Hoja tunayotaka kujenga hapa ni kwamba Serikali imefanya  makosa makubwa kuelekeza nguvu na rasilimali nyingi katika kutafuta tiba ya malaria badala ya kutafuta chanzo chake kwa kutokomeza mazalio ya mbu. Tumekuwa tukijidanganya kwa kudhani kwamba tutatokomeza ugonjwa huo kwa kusambaza vyandarua au  kubadilisha dawa za kutibu malaria. Inaonekana tunafanya hivyo makusudi au hatujui  kwamba gharama za kuzuia malaria ni ndogo mno kuliko gharama za kuitibu.
Katika miaka ya 80 Serikali ya Japan ilibuni na kufadhili mradi wa kunyunyizia dawa katika mazalio ya mbu hapa nchini. Hata hivyo, mradi huo ulihujumiwa kwa sababu uligusa masilahi ya wakubwa waliokuwa wakineemeka na uingizaji nchini wa dawa za kutibu malaria. Ndiyo maana ugonjwa wa malaria unaendelea kudunda na kusababisha maafa tuliyoyataja hapo juu.
Tunaambiwa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), limepanga kujenga kiwanda mkoani Pwani cha kutengeneza dawa za kuangamiza mazalio ya mbu. Jambo la ajabu ni kwamba mpango huo unapigwa vita kila kona kwa sababu unagusa masilahi ya kundi fulani. Badala yake, tunaambiwa Serikali inahaha huku na kule kuhakikisha sera na miongozo yake kuhusu tiba ya Malaria zinabadilishwa haraka ili dawa mpya ya Artesunate ianze kutumiwa mwezi huu badala ya Quinine. Bila shaka wanaofaidika na mradi huo watakuwa wakisema kimya kimya: ‘Udumu ugonjwa wa malaria’.
PIGA +255764043111 OR +255718832888 KWA KUTENGENEZEWA BLOG AU WEBSITE,COMPUTER TECHNICIAN AU KWA MAFUNZO YAHUSUYO COMPUTER BY JAMES KUZWA